TANGAZO LA DHARURA
KUZIMWA KWA MTAMBO WA UZALISHAJI MAJI RUVU JUU
14.04.2023
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) inawatangazia wateja na wananchi wanaohudumiwa na Mtambo wa kuzalisha maji Ruvu Juu kuwa, kutakuwa na ukosefu wa huduma ya maji kwa wastani wa saa 16 siku ya Jumamosi , Aprili 15, 2023.
Muda: Kuanzia Saa 12 jioni hadi Saa 4 asubuhi Jumapili
Sababu: Kuruhusu matengenezo ya bombakubwa la inchi 36 eneo la Visiga Saheni na kutoa matoleo mawili maeneo ya Kwembe na Msigani yanayolenga kuboresha upatikanaji wa huduma ya maji maeneo ya Kibamba Pangaboy na Mbezi Malamba Mawili.
Maeneo yatakayoathirika ni;
Chalinze, Chalinze Mboga, Msoga, Ruvu Darajani, Ruvu JKT, Vigwaza, Mlandizi, Mbwawa, Visiga, Maili 35, Misugusugu, Kongowe, Soga, Miembe Saba, Kwa Mfipa, Mwendapole, Tanita, Kwa Mathias, Kwa Mbonde, Picha ya Ndege, Lulanzi, Kibaha, Kiluvya, Kibamba, Mloganzila, Mbezi Magari Saba, Mbezi Kwa Yusufu, Njeteni, Msigani, Kifuru, Mbezi Inn, MbeziStendi ya Magufuli, Mbezi Mshikamano, Mbezi Louis, Makabe, Msakuzi, Mbezi, Kimara,Tabata, Segere, Kinyerezi, Kisukuru, Bonyokwa, Kimara B, Kimara Korogwe, Bucha, Baruti, Ubungo, Magomeni, Ukonga, Uwanja wa Ndege, Kiwalani, Vingunguti, Gongo la Mboto, Pugu na Kisarawe.
Tunaomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza.
Wasiliana nasi kupitia kituo cha huduma kwa wateja 0800110064 (bure) au
0735 202-121 (WhatsApp Tu)
Imetolewa na
Kitengo cha Mawasiliano na Jamii
DAWASA