Announcements

Posted On: Sep 20, 2022


TAARIFA KWA UMMA

KUKOSEKANA KWA HUDUMA YA MAJI KWA WAKAZI WA TEMEKE HADI KURASINI

20/09/2022

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar-es-salaam (DAWASA) inawatangazia wateja na wananchi wa Temeke hadi Kurasini kuwa kutakuwa na ukosefu wa huduma ya maji leo, Septemba 2022, kwa muda wa saa 6 kuanzia saa 5:00 asubuhi hadi 12:00 jioni

Sababu: Matengenezo katika bomba kuu la inch 15 katika eneo la Mbozi - Temeke.

Maeneo yatakayoathirika ni:-

Changombe, Mgulani, Magorofa ya jeshi, Uwanja wa taifa, Magurumbasi A&B, Mbozi, Mivinjeni, Keko, kurasani na baadhi ya maeneo ya kata ya Temeke.

Tunaomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza.

Wasiliana nasi kupitia kituo cha huduma kwa wateja 0800110064 (Bure)

0737-730523(DAWASA TEMEKE)

Imetolewa na

Kitengo cha Mawasiliano

DAWASA