Announcements

Posted On: Jul 16, 2021


TAARIFA KWA UMMA

KUKOSEKANA KWA UMEME KATIKA MTAMBO WARUVU JUU.

16.07.2021

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar-es-salaam (DAWASA) inapenda kuwajulisha wananchi wanaohudumiwa na Mtambo wa Uzalishaji Maji ya Ruvu Juu kuwa, kumekuwa na changamoto ya umeme hivyo kuathiri uzalishaji maji na kupelekea kukosekana kwahuduma kwenye maeneo yanayohudumiwa na mtambo huo kuanzia saa 3 asubuhi.

Sababu ya ukosefu wa majisafi Tatizo la umeme wa TANESCO kwenye mtambo wa uzalishaji maji Ruvu Juu.

Maeneo yatakayoathirika:

Mlandizi, Ruvu Darajani, Vikurutu, Visiga, Misugusugu, Kongowe, Soga, Maili 35, Kwa Mfipa, Mwenda Polepole, Kwa Mathias, Mkuza, Picha ya Ndege, Shirika la Elimu Kibaha, Pangani, Maili Moja, Kibaha, Kiluvya, Kibamba, Mbezi, Temboni, Kwa Msuguri, Saranga, Golani, Stop Over, Bonyokwa, Changanyikeni, Buguruni, Ubungo, Kisiwani, Msewe, Kilungule, Tabata, Segerea, Kinyerezi, Kiwalani, Pepsi mpaka Airport.

Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.

Kwa taarifa zaidi, wasiliana nasi kupitia kituo cha huduma kwa wateja 0800110064 au *152*00# (BURE)

IMETOLEWA NA

Kitengo cha Mawasiliano na Jamii

DAWASA