TAARIFA KWA UMMA
KUZIMWA KWA MTAMBO WA UZALISHAJI MAJI RUVU CHINI
21.9.2022
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) inawatangazia Wateja na wananchi wanaohudumiwa na mtambo wa kuzalisha maji Ruvu Chini kuwa Mtambo utazimwa siku ya ijumaa tarehe 23/9/2022 kuanzia saa 12 asubuhi mpaka saa 2 usiku
Sababu: Kuruhusu matengenezo makubwa ya bomba kuu maeneo ya Mlalakuwa na Mwenge.
Maeneo yatakayo athirika ni pamoja na; Bagamoyo, Zinga, Kerege, Mapinga, Mabwepande, Bunju, Tegeta, Mbweni, Boko, Salasala, Goba, Mivumoni, Kawe, Lugalo, Makongo, Chuo Kikuu, Mwenge, Kijitonyama, Mikocheni, Msasani, Oysterbay, Masaaki, Mwananyamala, Kinondoni, Hospitali ya Taifa Muhimbili, Magomeni, Kigogo, Chang'ombe, Keko, Kurasini, Kigamboni, Airport, Kiwalani, Buguruni,Kigamboni Vingunguti,Ilala na Katikati ya mji.
Tunaomba radhi kwa usumbufu utakaotokea.
Tafadhali kumbuka kuhifadhi maji ya kutosha ili kuwa na hifadhi ya kutosha kipindi cha matengenezo
Wasiliana nasi kupitia kituo cha huduma kwa wateja 0800110064 (bure) au
0735 202-121(WhatsApp tu)
Imetolewa na
Kitengo cha Mawasiliano
DAWASA