Announcements

Posted On: Apr 08, 2021


TAARIFA KWA UMMA

MATENGENEZO MTAMBO WA MAJI - RUVU JUU

8/4/2021

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar-es-salaam (DAWASA) inawataarifu Wananchi wanaohudumiwa na Mtambo wa maji Ruvu Juu kuwa kutakuwa na ukosefu wa huduma ya maji leo tarehe 8/ 4/2021.

Sababu ya ukosefu wa majisafi: Hitilafu kwenye mfumo wa umeme mtamboni

Maeneo yatakayoathirika: Mlandizi, Ruvu Darajani, Vikurutu, Visiga, Misugusugu, Kongowe, Soga, Maili 35, Kwa Mfipa, Mwenda Polepole, Kwa Mathias, Mkuza, Picha ya Ndege, Shirika la Elimu Kibaha, Pangani, Maili Moja, Kibaha, Kiluvya, Kibamba, Mbezi, Temboni, Kwa Msuguri, Saranga, Golani, Stop Over, Bonyokwa, Changanyikeni, Buguruni, Ubungo, Kisiwani, Msewe, Kilungule, Tabata, Segerea, Kinyerezi, Kiwalani, Pepsi mpaka Airport.

Jitihada za kutatua tatizo hilo zinaendelea.

Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.

Kwa taarifa zaidi, wasiliana nasi kupitia kituo cha huduma kwa wateja 0800110064 au *152*00# (BURE).

IMETOLEWA NA

Kitengo cha Mawasiliano na Jamii

DAWASA