Announcements

Posted On: Apr 01, 2021


TAARIFA KWA UMMA

MATENGENEZO YA BOMBA LA INCH48 VISIGA SAHENI

31/3/2021

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar-es-salaam (DAWASA) inatarajia kufanya matengenezo ya kuzuia uvujaji katikabomba la inchi 48 maeneo ya Visiga Saheni kesho Alhamisi tarehe 1/4/2021 kwa masaa 12 hadi 14 na kupelekea upungufu wa huduma ya maji.

Maeneo yatakayoathirika: Kwembe, Njeteni, Msingwa, Msigani, NatambuaMawili, Kwa Msuguri, Saranga, Kanisa la Udongo, Kilima cheupe, Golani, Kimara B, Tabata Segerea, Bonyokwa, Kinyerezi, Songas, Kifuru, Kibaga, Kiwalani, Pepsi, na Airport.

Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.

Kwa taarifa zaidi, wasiliana nasi kupitia kituo cha huduma kwa wateja 0800110064 au *152*00# (BURE).

IMETOLEWA NA

Kitengo cha Mawasiliano na Jamii

DAWASA