Announcements

Posted On: Jul 30, 2021


TAARIFA KWA UMMA

UKOSEFU WA HUDUMA YA MAJI KIBAMBA HADI KIMARA

30.7.2021

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) inawatangazia wateja na wananchi wa Eneo la Kibamba hadi Kimara kuwa kutakua na ukosefu wa huduma ya maji kwa saa 14 kuanzia saa 8 Mchana hadi saa 10 usiku tarehe 30.07.2021.

Sababu: Kuruhusu matengenezo ya bomba la 48" eneo la Kiluvya kwa Komba ili kuzuia upotevu wa maji.

Maeneo yatakayoathirika:

Njeteni, Mbezi Msigani, Malamba Mawili, Malamba Kanisani, Soweto kuelekea Kifuru, Kwa Musuguli, Saranga, Kimara Bonyokwa, Golan, Mbezi, Kibanda Cha Mkaa, Songas Plant, Kimara B, Kimara King'ongo na Kimara Bakery.

Tunaomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza

Wasiliana nasi kupitia kituo cha huduma kwa wateja 0800110064 (bure) au

0735 202121(WhatsApp tu)

Imetolewa na

Kitengo cha Mawasiliano na Jamii