Announcements

Posted On: Apr 22, 2022


TAARIFA KWA UMMA

UKOSEFU WA HUDUMA YA MAJI KWA WAKAZI WA VINGUNGUTI HADI BUZA

22. 04. 2022

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) inawataarifu wakazi wa maeneo ya Vingunguti hadi Buza Jijini Dar es salaam kuwa kutakuwa na ukosefu wa huduma ya maji kwa muda wa saa 12, siku ya Ijumaa 22 Machi kuanzia saa 9 alasiri hadi saa 9 usiku.

Sababu: Matengenezo ya bombal inchi 18 katika eneo la Mto Msimbazi liliosababishwa na hitilafu kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha

Maeneo yatakayoathirika ni Tabata eneo la viwanda, Chang'ombe, Kimanga, Barakuda, Vingunguti, Msimbazi, Liwiti, Sitakishari, Kipawa, Airport Terminal 3, Kiwalani, Pepsi, Ukonga Magereza na Buza

Tunaomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza

Wasiliana nasi kupitia kituo cha huduma kwa wateja 0800110064 (bure) au

0735 202-121(WhatsApp tu)

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano na Jamii

DAWASA