Announcements

Posted On: Aug 30, 2022


TAARIFA MUHIMU KWA WATEJA WA DAWASA MABADILIKO YA AKAUNTI NAMBA ZA WATEJA.

25.08.2022

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) imeanza rasmi kutumia mfumo wa ankara wa Serikali.

Kufuatia mabadiliko haya, tunawataarifu wateja wetu wote kwamba kutakuwa na mabadiliko kwenye nambari za akaunti.

Mabadiliko hayo yataanza kuonekana katika ankara ya mwezi Agosti 2022.

Akaunti namba zote sasa zitaanza na A104 na mteja atapokea namba mpya ya kumbukumbu itakayoanza na 99104 kwa ajili ya kufanya malipo.

Kwa maelezo zaidi, Tafadhali Piga 0800110064 (bure).

Imetolewa na
Kitengo cha Mawasiliano na Jamii

DAWASA