TAARIFA MUHIMU
ZOEZI LA USOMAJI MITA ZA MAJI KUANZA OKTOBA 10, 2023
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) inawataarifu Wateja wake kuwa zoezi la usomaji mita za maji litaanza Oktoba 10 - 15, 2023.
Mamlaka inaomba ushirikiano wa wateja wote wakati watoa huduma watakapokuwa wanapita kutekeleza zoezi hili.
Kumbuka baada ya zoezi hili wateja wataanza kupokea ujumbe wa ankara ya matumizi ya maji kupitia mawasiliano rasmi ya wateja.
Kwa taarifa zaidi wasiliana nasi kupitia kituo cha huduma kwa wateja 0800110064 (Bure) na 0735-202121 (WhatsApp tu)
Imetolewa na
Kitengo cha Mawasiliano
DAWASA