Photo Gallery

 • DAWASA TUNAWAFIKIA-MKURANGA

  Utekelezaji wa ujenzi wa Mradi wa maji Mji wa Mkuranga ukiendelea kwa kasi. Mradi huu unahusisha ujenzi wa tanki la maji la ujazo wa lita Milioni 1.5, ulazaji wa bomba za inchi 8 kwa umbali wa kilomita 63. Kukamilika kwa mradi huu kutahudumia wananchi takribani 25,500 wa maeneo ya Mkuranga A,Kiguza, Mgawa, Mkwalia, Kitumbo, Njia Nne, Sunguvuni na Oyoyo.

  Posted On : July, 03, 2020

 • DAWASA TUNAWAFIKIA

  Naibu Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso akiongea na wakazi wa eneo la Mbwawa ,mji wa Kibaha na kuwahakikishia kuwa tatizo la maji katika eneo litakwisha ndani ya siku 60. Mkutano huo unatokana na agizo la Rais John Pombe Magufuli alilotoa juni 28, 2020 wakati wa ziara yake.

  Posted On : July, 01, 2020

 • UZINDUZI WA MRADI WA MAJI WA KIBAMBA-KISARAWE

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizindua mradi wa Maji wa Kibamba-Kisarawe

  Posted On : July, 01, 2020

 • Watumishi DAWASA wachukua tahadhari

  Watumishi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) wakisafisha mikono kuhamasisha usafi binafsi na tahadhari dhidi ya magonjwa ya mlipuko hususani virusi vya Corona.

  Posted On : March, 17, 2020