Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Daniel Chongolo akipata ufafanuzi wa mradi wa usambazaji maji kuanzia Chuo Kikuu Dar es Salaam hadi Mji wa Bagamoyo Mkoa wa Pwani kutoka kwa Msimamizi wa Mradi wa DAWASA, Mhandisi Ishmael Kakwezi wakati wa ziara ya kukagua na kutambulisha mradi wa maji kwa watendaji wa kata na mitaa. Mradi huu utanufaisha wakazi wa maeneo ya Changanyikeni, Salasala, Kinzudi, Goba, Kibululu, Tegeta A, Mbopo, Nyakasagwe, Mivumoni, Madale, Wazo, Bunju, Mbweni, Mabwepande na Bagamoyo.
Posted On : September, 14, 2020
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Abubakar Kunenge akipata ufafanuzi wa ujenzi wa mradi wa maji wa usambazaji maji Chuo Kikuu Dar hadi Bagamoyo (Mkoa wa Pwani) kutoka kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja wakati wa ziara ya kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maji Jiji la Dar es salaam.
Utekelezaji wa ujenzi wa Mradi wa maji Mji wa Mkuranga ukiendelea kwa kasi. Mradi huu unahusisha ujenzi wa tanki la maji la ujazo wa lita Milioni 1.5, ulazaji wa bomba za inchi 8 kwa umbali wa kilomita 63. Kukamilika kwa mradi huu kutahudumia wananchi takribani 25,500 wa maeneo ya Mkuranga A,Kiguza, Mgawa, Mkwalia, Kitumbo, Njia Nne, Sunguvuni na Oyoyo.
Posted On : July, 03, 2020
Naibu Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso akiongea na wakazi wa eneo la Mbwawa ,mji wa Kibaha na kuwahakikishia kuwa tatizo la maji katika eneo litakwisha ndani ya siku 60. Mkutano huo unatokana na agizo la Rais John Pombe Magufuli alilotoa juni 28, 2020 wakati wa ziara yake.
Posted On : July, 01, 2020
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizindua mradi wa Maji wa Kibamba-Kisarawe
Watumishi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) wakisafisha mikono kuhamasisha usafi binafsi na tahadhari dhidi ya magonjwa ya mlipuko hususani virusi vya Corona.
Posted On : March, 17, 2020