Matangazo

Imewekwa: May 19, 2021


TAARIFA KWA UMMA

MATENGENEZO MTAMBO WA UZALISHAJI MAJI RUVU JUU

19/5/2021

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar-es-salaam (DAWASA), inawatangazia Wananchi na wateja wake wote wa Kibaha na Mlandizi mkoani Pwani wanaohudumiwa na mtambo wa uzalishaji maji wa Ruvu Juu, kuwa huduma ya majisafi itakosekana kwa muda wa saa 12 kwa siku ya Jumatano tarehe 19.05.2021

Sababu: Hitilafu iliyojitokeza kwenye pampu za kuchota Maji na zile za kusafirisha Majighafi katika Mtambo wa wa Ruvu Juu.

Maeneo yatakayoathirika ni pamoja na:-

Mlandizi Mjini, Ruvu Darajani, Vikuruti, Disunyara, Kilangalanga, Janga, Mbagala, Visiga, Maili 35, Zogowale, Misugusugu, Tanita, Kibondeni, Kwa Mathias, Nyumbu, Msangani, Kwa Mbonde, Picha Ya Ndege, Sofu, Lulanzi, Gogoni, Kibamba, Kibamba Njia Panda Shule Kibwegere, Mloganzira, Kwembe, Kibamba Hospitali, Kwa Mkinga, Luguruni, Mbezi, Kimara, Ubungo, Makongo, Tabata, Bonyokwa, Kinyerezi, Kisukuru, Kipawa na Kiwalani.

Mafundi wanaendelea na jitihada za kurekebisha hitilafu iliyojitokeza ili huduma irejee.

DAWASA inaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.

Wasiliana nasi kupitia kituo cha huduma kwa wateja 0800110064 (BURE) na 0735202121 (WhatsApp tu).

Imetolewa na:

Idara ya Mawasiliano na Jamii

DAWASA