Matangazo

Imewekwa: Jun 07, 2021


TAARIFA KWA UMMA

UKOSEFU WA HUDUMA YA MAJI MWANANYAMALA HADI KATIKATI YA MJI

7/6/2021

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar-es-salaam (DAWASA) inapenda kuwataarifu wananchi na wakazi wa maeneo ya Mwananyamala hadi Katikati ya Mji kuwa kutakuwa na ukosefu wa huduma ya majisafi kwa muda wa saa 8 kwa siku ya tarehe 07/06/2021.

Sababu: Matengenezo ya miundombinu ya bomba la inchi 18 katika eneo la Morocco-kinondoni ili kupisha upanuzi wa barabara.

Maeneo yatakayoathirika ni Mwananyamala, Makumbusho, Msasani, Masaki, Oysterbay, kivukoni na Katikati ya Mji

DAWASA inaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.

Wasiliana nasi kupitia kituo cha huduma kwa wateja 0800110064 na

0735 202121(whatsap tu)

Imetolewa na:

Kitengo cha Mawasiliano na Jamii