PUMZIKA KWA AMANI
21 Oct, 2026
Pakua
PUMZIKA KWA AMANI
DANIEL GODFREY ITAJA
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) anasikitika kutangaza kifo cha mtumishi wa Mamlaka Ndg. Daniel Godfrey Itaja (Fundi Msaidizi - DAWASA Kibaha) kilichotokea siku ya Jumatatu tarehe 19 Oktoba, 2026 saa 01:20 Usiku kwa Ajali.
Kwa sasa msiba upo nyumbani kwa Mjomba wa Marehemu - Mbezi Beach Jogoo, Dar es Salaam.
DAWASA inaungana na familia ya marehemu katika kuomboleza msiba huu mzito.
Taarifa zaidi kuhusu taratibu za mazishi zitaendelea kutolewa kwa kadri tutakavyopokea kutoka kwa Familia.
Bwana Alitoa, Bwana Ametwaa, Jina la Bwana Libarikiwe
