Wizara ya Maji

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA)

TIRA Logo
Jinsi ya Kulipia Bili ya DAWASA

Jinsi ya Kulipia Bili ya DAWASA

DAWASA inawapatia wateja njia rahisi na salama za kulipia bili ya maji kupitia mitandao ya simu na benki kwa kutumia Control Number iliyopo kwenye bili yako ya maji.


1. Malipo Kupitia Mitandao ya Simu

Vodacom M-Pesa

  1. Piga *150*00#

  2. Chagua 4 – Lipa Bili

  3. Chagua 5 – Malipo ya Serikali

  4. Weka Control Number ya DAWASA

  5. Weka Kiasi cha Malipo

  6. Thibitisha kwa kuweka Namba ya Siri (PIN)

  7. Utapokea SMS ya uthibitisho wa malipo


Mixx by Yas

  1. Piga *150*01#

  2. Chagua 4 – Lipa Bili

  3. Chagua 5 – Malipo ya Serikali

  4. Weka Control Number ya DAWASA

  5. Weka Kiasi cha Malipo

  6. Thibitisha kwa kuweka Namba ya Siri (PIN)


Airtel Money

  1. Piga *150*60#

  2. Chagua 5 – Lipa Bili

  3. Chagua 4 – Malipo ya Serikali

  4. Weka Control Number ya DAWASA

  5. Weka Kiasi cha Malipo

  6. Thibitisha kwa kuweka Namba ya Siri (PIN)


T-Pesa

  1. Piga *150*71#

  2. Chagua 4 – Lipa Bili

  3. Chagua 5 – Malipo ya Serikali

  4. Weka Control Number ya DAWASA

  5. Weka Kiasi cha Malipo

  6. Thibitisha kwa kuweka Namba ya Siri (PIN)


HaloPesa

  1. Piga *150*88#

  2. Chagua 4 – Lipa Bili

  3. Chagua 5 – Malipo ya Serikali

  4. Weka Control Number ya DAWASA

  5. Weka Kiasi cha Malipo

  6. Thibitisha kwa kuweka Namba ya Siri (PIN)


2. Malipo Kupitia Benki

Wateja wanaweza pia kulipia bili ya maji kupitia matawi ya benki au huduma za benki kwa simu (Mobile Banking / Internet Banking).

Hatua za Kufanya Malipo

  1. Tembelea tawi la benki yoyote au fungua Mobile Banking / Internet Banking.

  2. Chagua Bill Payment / Lipa Bili.

  3. Chagua Malipo ya Serikali (Government Payments).

  4. Weka Control Number ya DAWASA.

  5. Weka Kiasi cha Malipo.

  6. Thibitisha malipo na uhifadhi risiti au ujumbe wa uthibitisho.


Taarifa Muhimu kwa Wateja

  • Hakikisha umeweka Control Number sahihi.

  • Hifadhi SMS au risiti ya malipo kama uthibitisho.

  • Malipo yanaweza kuonekana kwenye mfumo wa DAWASA ndani ya dakika chache baada ya kukamilika.