Wizara ya Maji

Dar es Salaam Water Supply And Sanitation Authority (DAWASA)

TIRA Logo
DAWASA NA WADAU WAKUTANA KUBORESHA HUDUMA
07 Oct, 2024
DAWASA NA WADAU WAKUTANA KUBORESHA HUDUMA

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) imetembelea wateja wakubwa, Taasisi za Serikali na Mashirika binafsi Wilaya ya Kigamboni kwa lengo la kuboresha huduma kubaini changamoto zao ili kuongeza ufanisi katika  kuhudumia jamani.

Akizungumza wakati alipotembelea wateja wakubwa katika Kata ya Feri, Afisa Mawasiliano DAWASA ndugu Jamil Bakari ameeleza lengo ni kuboresha uhusiano na kua karibu zaidi na wateja hao ili kuimarisha huduma bora wanayopatiwa.

"Tumeweza kutembelea baadhi ya Taasisi za Umma na Mashirika binafsi, tunayo furaha kuona wateja wengi wanaridhika na huduma yetu, tumepokea ushauri pia ambao tutaenda kuufanyia kazi" ameeleza ndugu Jamil.

Kwa upande wake ndugu, Wema Golungwa kutoka kampuni ya Manjis ameishukuru DAWASA kwa kutoka na kuja kusikiliza na kupata maoni ya huduma kutoka kwa wateja wao, kwani jambo hilo litachochea zaidi mahusiano baina ya DAWASA na wateja wake kitendo kitchopelekea huduma kuwa bora.

Baadhi ya wateja wakubwa waliotembelewa ni pamoja na Hospital ya Wilaya, Tipper Company,Oryx, Chuo cha Mwalimu Nyerere, Kampuni ya Manjis, Kikosi cha Ujenzi pamoja na TAFICO.