Wizara ya Maji

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA)

TIRA Logo
WAZIRI AWESO AENDELEA NA ZIARA KUFUATILIA HALI YA MAJI DAR, AKAGUA TENKI LA KISANGA
08 Dec, 2025
WAZIRI AWESO AENDELEA NA ZIARA KUFUATILIA HALI YA MAJI DAR, AKAGUA TENKI LA KISANGA

Waziri wa Maji, Mheshimiwa Jumaa Aweso (Mb) ameendelea na ziara yake ya kukagua na kufatilia hali ya maji katika mitaa mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam ambapo asubuhi ya leo Jumatatu 8.12.2025 amefika katika tenki la kuhifadhi maji Kisanga kushuhudia ujazaji wa tenki hilo pamoja na usambazaji kwa wananchi.

Waziri Aweso amewataka watendaji wa DAWASA kuwa mitaani na kufatilia hali ya usambazaji wa maji ili kila mwananchi apate maji na wale wenye changamoto za kutofikiwa na huduma kutatuliwa kwa wakati.

"Tumeona tenki lina maji ya kutosha, kazi inayoendelea ni kusambazwa kwa maji haya yanayopatikana ili kila mwananchi apate kwa usawa, tunatambua hali tunayopitia kwasasa ni ya mpito lakini lazima tupambane wananchi wapate huduma ya maji," amesema Mheshimiwa Aweso.

Ndugu Felista Michael, Mkazi wa Tegeta kwa Ndevu ameshukuru jitihada za watendaji wa Wizara ya Maji wakiongozwa na Waziri wa Maji, Mheshimiwa Jumaa Aweso kufatilia hali ya maji na kuhakikisha wanapata huduma, huku akiwasihi wananchi wenzake kutunza maji haya wanapoyapata mpaka pale hali itakapokaa sawa.

Wananchi wa maneno ya Tegeta, Bahari beach, Msichoke, Kunduchi NDC, Kyaroni, Mecco, Mtongani, Skanska, Madini, Maputo, Mtakuja, Kunduchi Pwani, Rafia na Kilongawima wanaendelea kupata huduma ya majisafi mara baada ya kujazwa kwa tenki la Kisanga lililopo kata ya Wazo.