Wizara ya Maji

Dar es Salaam Water Supply And Sanitation Authority (DAWASA)

TIRA Logo
DAWASA NYUMBA KWA NYUMBA KUHAMASISHA MAKUSANYO KISARAWE
09 Dec, 2024
DAWASA NYUMBA KWA NYUMBA KUHAMASISHA MAKUSANYO KISARAWE

Watumishi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) Mkoa wa Kihuduma wa Kisarawe wanaendelea na zoezi la makusanyo kwa ufuatiliaji wa malipo ya huduma za maji kwa wateja wenye madeni ya bili za maji nyumba hadi nyumba katika maeneo ya kihuduma.

Zoezi hili linaendelea kutekelezwa katika mitaa mbalimbali ya kimkoa ikiwemo Bomani, Umatumbini, Sanze, Chanzige, Pugu na Kimani huku likienda sambamba na utoaji wa elimu ya matumizi sahihi ya maji, utunzaji wa vyanzo vya maji, ulinzi wa miundombinu ya maji, umuhimu wa kulipa bili za maji kwa wakati pamoja na kusitisha huduma kwa wateja wenye malimbikizo ya madeni ya bili.

Mamlaka inasisitiza wananchi na wateja wa DAWASA katika maeneo yote ya kihuduma kulipa bili zao kwa wakati ili kuepukana na usumbufu wa kusitishiwa huduma kutokana na bili kutolipa kwa wakati.