DAWASA YAWEKA KAMBI MTUNGI WA MAJI - MKURANGA KUFUATILIA HUDUMA
09 Jul, 2024

Mafundi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) Mkoa wa kihuduma Mkuranga wameweka kambi katika mtaa wa Mtungi katika Kata ya Mipeko kwa lengo la kubaini chanzo cha ukosefu wa huduma ya Maji kwa baadhi ya wakazi.
Mamlaka inaendelea na jitihada za makusudi kuhakikisha inarejesha huduma katika hali ya kawaida kwa wakazi takribani 400 katika mtaa wa Poti kata ya Mipeko wilaya ya Mkuranga.