GOBA WAITWA MAUNGANISHO MAPYA HUDUMA YA MAJISAFI

Wananchi wapongeza utoaji vifaa vya maunganisho mapya.
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) imeendesha zoezi la utoaji wa vifaa vya maunganisho mapya kwa wakazi 88 waliokamilisha taratibu za maunganisho ya huduma ya Majisafi katika maeneo yanayohudumiwa na mkoa wa kihuduma DAWASA Makongo.
Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa vya maunganisho mapya ,Afisa Huduma kwa Wateja Negwako Aron ameeleza kuwa Mamlaka imekabidhi vifaa kwa wateja 88 kutoka maeneo ya Goba, Tegeta A, Matosa, Mbezi Luis, Makongo Juu na Kilungule ikiwa ni hatua endelevu ya Mamlaka ya kufikisha huduma bora kwa kila mwananchi na huduma inakuwa bora.
"Leo sisi kama DAWASA Makongo tuko hapa kwa kazi moja ya kutekeleza adhma yetu kama Mamlaka ya kusogeza huduma kwa kila mwananchi ambapo tumekabidhi vifaa vya maunganisho mapya ikiwa ni muendelezo wa uboreshaji wa huduma yetu." ameeleza
Ndugu Negwako amewakumbusha Wananchi ambao wamepokea vifaa vya maunganisho mapya leo kukumbuka wajibu wa mteja ambao ni kutunza miundombinu ya Maji, kutumia huduma ya Maji kwa usahihi na kulipia bili za maji kwa wakati ili kuiwezesha Mamlaka kutoa huduma endelevu.
Ndugu Mwanamkuu Mohammed mkazi wa Goba amepongeza juhudi za DAWASA kuwapatia vifaa vitakavyowawezesha kunufaika na huduma ya maji huku mategemeo na kuwa chachu katika shughuli za kijamii na uchumi.