Wizara ya Maji

Dar es Salaam Water Supply And Sanitation Authority (DAWASA)

TIRA Logo
KAIMU MTENDAJI MKUU DAWASA AANZA ZIARA KUZUNGUMZA NA WATUMISHI
19 Dec, 2024
KAIMU MTENDAJI MKUU DAWASA AANZA ZIARA KUZUNGUMZA NA WATUMISHI

Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Mkama Bwire ameanza ziara yake ya siku ya kwanza kwa kukutana na Watumishi wa Mikoa ya Kihuduma DAWASA Ruvu Chini, Bagamoyo, Mapinga, Mabwepande na Mivumoni kwa lengo la kuwasikiliza na kuimarisha mahusiano mahala pa kazi .

Katika ziara yake ameambatana na Viongozi waandamizi wa Mamlaka  pamoja na wawakilishi wa vyama vya Wafanyakazi ikiwa ni ahadi yake aliyoitoa ya kukutana na Watumishi ili kujadiliana namna bora ya kuhakikisha huduma bora ya Majisafi na Usafi wa Mazingira inawafikia Wananchi wa Dar es salaam na Pwani.

“Nguvu kubwa yetu sisi (Watumishi) ni Wateja, tukaongeze jitihada kwenda kuwahudumia na kusikiliza changamoto zao ili kwa pamoja tufikie malengo yetu ya usambazaji huduma yenye viwango na kwa Wateja” alisisitiza Mhandisi Bwire.