MABORESHO MFUMO WA UMEME MTAMBO WA RUVU JUU MBIONI KUKAMILIKA, HUDUMA KUREJEA.

Kazi ya Maboresho ya mfumo wa umeme unaoendesha Pampu za kusukuma maji katika mtambo wa uzalishaji maji Ruvu Juu kutekelezwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) kwa kushirikiana na Shirika la umeme Tanzania (TANESCO) iko mbioni kukamilika ili kuimarisha huduma ya Maji katika maeneo ya Kibaha hadi Kisaware.
Kumalizika kwa kazi hii kutaimarisha upatikanaji wa Maji kwa Wananchi katika maeneo ya
Ruvu Darajani, Ruvu JKT, Vigwaza, Mlandizi, Mbwawa, Visiga, Maili 35, Misugusugu, Kongowe, Soga, Miembe Saba, Kwa Mfipa, Mwendapole, Tanita, Kwa Mathias, Kwa Mbonde, Picha ya Ndege, Lulanzi, Kibaha, Kiluvya, Kibamba, Mbezi, Magari Saba, Mbezi Inn, Mbezi Kimara, Tabata Segerea, Kinyerezi, Kisukuru, Bonyokwa, Msigani, Maramba Mawili, Kimara B, Kimara Korogwe, Bucha, Baruti, Ubungo, Magomeni, Ukonga, Uwanja wa Ndege, Kiwalani, Vingunguti, Gongo la Mboto, Pugu na Kisarawe.
Maboresho haya yanatarajia kukamilika leo Oktoba 21,2024.