MABORESHO YA MIUNDOMBINU YA MAJI PORI LA JESHI KIMARA

Kazi ya kudhibiti upotevu wa maji katika bomba la usambazaji maji la inchi 6 eneo la Pori la Jeshi Kimara Mavurunza imetekelezwa na mafundi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA)
Kazi hiyo imehusisha kubadilisha na kuchomelea bomba la plastiki ngumu (HDPE) katika sehemu iliyoathiriwa na mvua kwa lengo la kuboresha huduma ya upatikanaji maji katika maeneo yanayohudumiwa na bomba hilo.
Kukamilika kwa kazi hii kutarejesha huduma kwa wakazi wa maeneo ya;
Changanyikeni, Mbuyuni, DTV, Chuo cha Ardhi, Midizini, Njia Panda Jeshini, Mashine, Area four, Jeshini area A, Songasi, KKKT Makongo, Kanisa la Sabatho, Makongo Shule ya Msingi, Makongo Zahanati, Makongo Njia Panda DTV Matangini, Kwa salema, Kam Collage, Mavurunza, Makanisa Mawili, Golani, Matete, Ebonite na Kwa Mjata.