MATENGENEZO BOMBA KUBWA PUGU MBIONI KUKAMILIKA

Kazi ya matengenezo yanayohusisha kudhibiti uvujaji katika Bomba la inchi 6 kwa umbali wa Mita 24 pamoja na kujengea nguzo za zege ili kuimarisha kingo za bomba hilo katika eneo la Pugu njia panda ya Pinda iko katika hatua za mwisho kukamilika.
Kazi hiyo inayotekelezwa na Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) ilianza kutekelezwa Oktoba 1, 2024 na inatarajiwa kukamilika leo Oktoba 2, 2024.
Kwa sasa kazi inayoendelea ni kurudishia udongo katika eneo hilo lililochimbwa na itakapokamilika maji yatafunguliwa kwenda kwa wateja takribani 6,000 wa maeneo ya Pugu Bombani, Kigogo Fresh A na B, Relini Magnus, Mustafa, Kinyamwezi, Mgeule, Mgeule juu, Taliani, Nyeburu, Pugu Kajiungeni, Mwakanga, Buyuni, Kwa Mbiki, Kwa Zoo, Zavala, Dampo, na Chikila.
Kwa changamoto ya kihuduma wasiliana nasi kupitia
Kituo cha Huduma kwa Wateja 0800110064 (Bure)
0735 202121 (whatsap tu)
0738 096085 (Huduma kwa Wateja DAWASA Kisarawe)
Imeandaliwa na
Kitengo cha Mawasiliano
DAWASA