TAARIFA KWA UMMA
26 Mar, 2024
Pakua
TAARIFA KWA UMMA
KUANZA USOMAJI MITA ZA MAJI MWEZI APRILI 2024
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) inawataarifu wateja na wananchi katika mikoa ya Dar es Salaam na Pwani, kuwa zoezi la usomaji wa mita za maji utaanza Aprili 10 hadi 15, 2024.
Mamlaka inaomba ushirikiano kwa watoa huduma wa DAWASA pindi watakapopita katika makazi yenu kutekeleza zoezi hili.
Baada ya mita kusomwa, mteja atapokea ujumbe mfupi kwa simu ili kuhakiki usomaji kabla ya bili yake kutoka.
Kwa taarifa zaidi wasiliana nasi kituo cha huduma kwa wateja 0800110064 (Bure) na 0735-202121 (WhatsApp tu)
Imetolewa na
Kitengo cha Mawasiliano
9.4.2024