Wizara ya Maji

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA)

TIRA Logo
JE UNAHITAJI HUDUMA YA MAJI KUTOKA DAWASA?
14 Jul, 2025 Pakua
JE UNAHITAJI HUDUMA YA MAJI KUTOKA DAWASA?

JE UNAHITAJI HUDUMA YA MAJI KUTOKA DAWASA?

A) Fika Ofisi za DAWASA zilizo karibu nawe ukiwa na nyaraka zifuatazo;

1. Barua ya utambulisho wa makazi kutoka Serikali ya mtaa unapoishi

2. Picha mbili ndogo (Passport size)

3. Kitambulisho cha muombaji (iwe Kitambulisho kimojawapo kati ya hivi, kitambulisho cha Taifa, hati ya kusafiria, leseni ya gari au Kitambulisho cha mpiga kura)

B. Hatua inayofuata baada ya kupeleka nyaraka:

1. Utapewa fomu ya kuomba huduma ya muunganisho mpya ya huduma ya maji.

2. Ndani ya siku saba za kazi mtalaamu atafika nyumbani kwako kutoka DAWASA kwa ajili ya usanifu (survey) vipimo kwa ajili ya kuandaa gharama.

3. Utapokea gharama sambamba na kumbukumbu ya malipo kwa vifaa vya muunganisho mpya wa huduma ya Majisafi.

Kumbuka malipo ya muunganisho wa huduma ya maji (New Connection) hufanyika kupitia Benki Washirika na kupitia mitandao ya simu (usitoe fedha mkononi).

Baada ya malipo ya muunganisho wa huduma ya maji utapatiwa vifaa utaandaliwa na DAWASA na mteja kuunganishiwa huduma ya maji.