Wizara ya Maji

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA)

TIRA Logo
SIKU YA WANAWAKE DUNIANI: DAWASA TUTAZUIA MIVUJO YA MAJI MITAANI
09 Mar, 2026
SIKU YA WANAWAKE DUNIANI: DAWASA TUTAZUIA MIVUJO YA MAJI MITAANI

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imeungana na Wanawake Dunian kote katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika Kata ya Mburahati, Wilaya ya Ubungo, Mkoa wa Dar es salaam huku ikisisitiza ujumbe wa jamii kudhibiti upotevu wa maji. 

Maadhimisho haya yenye Kauli Mbiu,"Haki na Usawa kwa Wanawake na Wasichana: Msingi Jumuishi Kufikia Dira 2050" Serikali imelenga kusimamia dira hii jumuishi kusimamia haki na usawa kwa wanawake katika nyanja mbalimbali. 

Akizungumza katika maadhimisho hayo, mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam (RC), Mheshimiwa Albert Chalamila amesema Serikali inaangalia msingi mkubwa wa kauli mbiu kwa kuwaimarisha wanawake kiuchumi na kuwapa kipaumbele kwenye fursa mbali mbali. 

Naye Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala DAWASA, Bi Benadetha Mwabusila amesema kuelekea maadhimisho ya Siku ya Wanawake duniani, DAWASA wamelenga kuhakikisha wanamtua mama ndoo kichwani kwa kuhakikisha upatikanaji wa huduma ya Maji sambamba na kupunguza kiasi cha Maji kinachopotea.

“Changamoto yetu ya sasa ambayo tunahitaji ushirikiano na jamii ni upotevu wa Maji, DAWASA tunasema Kila tone la maji lina thamani, haachwi mtu hivyo tuwaombe Wananchi kutoa taarifa wanapoona mivujo ya maji kwa DAWASA” alisema Mwabusila