NAMNA YA KUWASILISHA MALALAMIKO AU KUTOA TAARIFA DAWASA
							
							
							
							
							
						
					
                            
                                 08 Nov, 2024
                            
                                                        
                                 Pakua
                            
                                                    
                    NAMNA YA KUWASILISHA MALALAMIKO AU KUTOA TAARIFA DAWASA
Ndugu mteja, DAWASA inapokea na kushughulikia malalamiko kuhusu utoaji wa huduma. Mteja anaweza kuwasilisha malalamiko yake kwa kutumia njia zifuatazo;
1. Fika katika Ofisi ya Huduma kwa wateja (DAWASA)
2. Kuandika Barua pepe (info@dawasa.go.tz) au barua kwa Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu.
3. Kupiga simu bure yenye nambari 0800110064.
4. Kuweka kwenye makundi mbalimbali ya WhatsApp yaliyoanzishwa na ofisi za DAWASA maeneo tofauti tofauti yakiwaunganisha Wateja wanaoishi katika eneo husika.
Chanzo: MKATABA WA HUDUMA KWA WATEJA 2024, KIFUNGU NAMBA 15 NA 16
            