NYARAKA MUHIMU ZA KUAMBATANISHA WAKATI WA KUOMBA HUDUMA YA MAJISAFI
NYARAKA MUHIMU ZA KUAMBATANISHA WAKATI WA KUOMBA HUDUMA YA MAJISAFI
Ili kuunganishia huduma ya Majisafi, mteja anapaswa kukamilisha hatua zifuatazo:-
1. Kujaza fomu ya maombi ya kuunganishwa kwenye huduma ya majisafi, fomu hii
inapatikana katika ofisi za DAWASA au tovuti ya DAWASA.
2. Mteja atawasilisha nakala ya nyaraka za uthibitisho wa umiliki wa eneo linalohitaji huduma ikiemo mkataba a mauzo ya kiwanja au hati ya nyumba
au kiwanja.
3. Ikiwa vyote viwili havipo, mombaji atapaswa kupata barua ya utambulisho
kutoka Serikali ya Mtaa anapoishi kuthibitisha umiliki wake wa eneo.
4. Ikiwa mwombaji anaishi nyumba ya kupanga, atapaswa kuwasilisha mkataba wake wa upangaji na barua ya mmiliki wa nyumba.
5. Mteja atatakiwa kuambatanisha kwenye nyaraka zake picha ndogo (passport size) mbili (2) na nakala ya kitambulisho cha Taifa.
6. Mteja atafanyiwa vipimo (survey) na kupatiwa gharama za malipo ya vifaa vya kuunganishiwa huduma ya maji.
7. DAWASA haitapoke fedha za maunganisho mapya endapo kukatokea upungufu
wa vifaa.
8. Endapo mteja atakuwa tayari kulipia gharama za maunganisho mapya wakati amepewa taarifa ya upungufu wa vifaa atatakiwa kukubali kwa maandishi
kusubiri vifaa pasipo kuleta usumbufu au kudai fidia DAWASA.