Wizara ya Maji

Dar es Salaam Water Supply And Sanitation Authority (DAWASA)

TIRA Logo
PUMZIKA KWA AMANI
13 Apr, 2025 Pakua
PUMZIKA KWA AMANI

PUMZIKA KWA AMANI

Eng. Gissima Nyamo-Hanga, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania

Menejimenti na Watumishi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mhandisi Boniface Gissima Nyamo-Hanga pamoja na dereva wake kilichotokea Mkoani Mara, Aprili 13, 2025.

Mhandisi Nyamo-Hanga alikuwa kiongozi shupavu, Mzalendo, anayefikika muda wote na mwenye maono makubwa katika kuleta mapinduzi ya kiufundi na huduma bora za umeme kwa Watanzania. Uongozi wake uliakisi uadilifu, weledi na uzalendo wa dhati kwa nchi yetu.

DAWASA inatoa pole kwa Familia ya marehemu, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, uongozi wa TANESCO pamoja na Watanzania wote waliguswa na msiba huu mkubwa. 

Tunaungana nanyi katika kipindi hiki kigumu na tunawaombea Marehemu Mwenyezi Mungu azipokee roho zao mahali pema peponi.

Pumzika kwa amani Mhandisi Gissima Nyamo-Hanga.
Umetangulia, lakini mchango wako utaishi milele.