SALAMU ZA MWAKA MPYA 2026
SALAMU ZA MWAKA MPYA 2026
Mimi Mhandisi Mkama Bwire, Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA), ninaungana na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuwatakia Heri ya Mwaka Mpya 2026 wadau wote wa huduma za Maji katika Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani.
DAWASA iko pamoja nayi, tunasikiliza sauti zenu na tunachukua hatua ili kuboresha huduma kwa ufanisi sambamba na kuendeleza miradi ya kimkakati ya Majisafi na Usafi wa Mazingira ndani ya eneo la kihuduma la DAWASA.
Tunaendelea kuboresha mifumo ya usimamizi wa utoaji huduma, ubunifu katika matumizi ya teknolojia sambamba na kuongeza uwazi na uwajibikaji, kuimarisha upatikanaji wa maji wa uhakika, pamoja na huduma rafiki kwa mteja kwa kuzingatia utu na viwango bora.
HERI YA MWAKA MPYA WA 2026
