TAARIFA KWA UMMA - KUANZA KWA ZOEZI LA USOMAJI MITA ZA MAJI
10 Jul, 2025
Pakua

TAARIFA KWA UMMA
KUANZA KWA ZOEZI LA USOMAJI MITA ZA MAJI
10.7.2025
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) inawaatarifu Wateja na Wananchi katika Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani, kuwa zoezi la usomaji mita za maji limeanza Julai 10 hadi 15, 2025.
Baada ya zoezi la usomaji mita kukamilika, Mteja atapokea ujumbe wa kuhakiki usomaji wa mita yake kabla ya bili kutumwa.
Kwa taarifa zaidi wasiliana nasi kituo cha huduma kwa wateja 0800110064 (Bure) na 0735 202121 (WhatsApp tu)
Imetolewa na
Kitengo cha Mawasiliano