TAARIFA KWA UMMA - KUANZA USOMAJI MITA ZA MAJI DAR ES SALAAM NA PWANI
10 Oct, 2025
Pakua
TAARIFA KWA UMMA
KUANZA USOMAJI MITA ZA MAJI DAR ES SALAAM NA PWANI
10.10.2025
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) inawaatarifu Wateja na Wananchi katika Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani, kuwa zoezi la usomaji mita za maji litaanza Oktoba 10 hadi 15, 2025.
Baada ya zoezi la usomaji mita kukamilika, Mteja atapokea ujumbe wa kuhakiki usomaji wa mita yake kabla ya bili kutumwa.
Kwa taarifa zaidi wasiliana nasi kupitia Kituo cha huduma kwa wateja 181 (Bure) na 0735 202121 (WhatsApp tu)
Imetolewa na
Kitengo cha Mawasiliano
