Wizara ya Maji

Dar es Salaam Water Supply And Sanitation Authority (DAWASA)

TIRA Logo
TAARIFA KWA UMMA - KUFUNGULIWA KWA DIRISHA LA UTOAJI VIFAA VYA MAUNGANISHO YA HUDUMA ZA MAJI
13 Jul, 2024 Pakua

TAARIFA KWA UMMA

KUFUNGULIWA KWA DIRISHA LA UTOAJI VIFAA KWA MAUNGANISHO YA HUDUMA ZA MAJI

Je, wewe ni mkazi wa Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani ambaye umeomba huduma ya maji na kukamilisha taratibu zote? 

Habari njema ni kuwa, Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) inawataarifu Wananchi wa maeneo yake ya kihuduma katika Mikoa wa Dar es Salaam na Pwani kuwa imeanza zoezi la utoaji wa vifaa kwa ajili ya maunganisho mapya ya huduma ya maji.

Pia Mamlaka inawakumbusha Wananchi waliokwisha kuomba huduma na kupigiwa simu na DAWASA, kufika katika ofisi zetu za kihuduma zilizopo maeneo mablimbali ili kupatiwa vifaa vya maunganisho. 

Kwa taarifa zaidi wasiliana nasi kupitia kituo cha huduma kwa wateja 0800110064 (Bure) na 0735 202 121 (WhatsApp tu) 

Imetolewa na 
Kitengo cha Mawasiliano