TAARIFA KWA UMMA - KUZIMWA KWA MTAMBO WA RUVU JUU KURUHUSU MATENGENEZO MUHIMU
							
							
							
							
							
						
					
                    TAARIFA KWA UMMA
KUZIMWA KWA MTAMBO WA RUVU JUU KURUHUSU MATENGENEZO MUHIMU
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) inawatangazia Wateja na Wananchi wanaohudumiwa kupitia Mtambo wa kuzalisha Maji Ruvu Juu uliopo Mlandizi Mkoani Pwani kuwa, kutakuwa na ukosefu wa huduma ya maji kwa muda wa saa 15, Septemba 4,2025 kuanzia Saa 12 asubuhi hadi Saa 3 usiku.
Sababu: Kuruhusu maboresho muhimu katika bomba kuu la kusafirisha Majighafi (Raw water) eneo la Mlandizi.
Maeneo yanayoathirika ni; 
Ruvu darajani, Ruvu JKT, Mlandizi, Mbwawa, Visiga, Mile 35, Misugusugu, Kongowe, Soga, Miembe Saba, Kwa Mfipa, Mwendapole, Tanita, Kwa Mathias, Kwa Mbonde, Picha ya Ndege, Lulanzi, Kibaha, Kiluvya, Kibamba, Mbezi, Magari Saba, Mbezi Inn, Mshikamano, Mbezi, Kimara, Kimara B, Kimara Korogwe, Bucha, Baruti, Ubungo, Makoka, Tabata, Kinyerezi, Kisukuru, Segerea, Msigani, Maramba Mawili, Vingunguti, Gongo la Mboto, Ukonga, Uwanja wa Ndege, Majumba sita, Kiwalani, Pugu na Kisarawe
Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.
Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kupitia kituo cha huduma kwa wateja 0800110064 (Bila Malipo) na 0735 202 121(WhatsApp tu)
Everlasting Lyaro
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano
DAWASA
            