TAARIFA KWA UMMA - OFA MAALUM YA KURUDISHIWA HUDUMA YA MAJI BILA KULIPA FAINI

TAARIFA KWA UMMA
OFA MAALUM YA KURUDISHIWA HUDUMA YA MAJI BILA KULIPA FAINI
9.05.2025
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) inapenda kuwajulisha Wananchi na wateja wake kuwa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kupitia Wizara ya Maji imetoa ofa maalum kuondoa faini ya kurejeshewa huduma (reconnection fee) kwa Wateja wanaodaiwa na Mamlaka ya Maji Nchini.
DAWASA inawataarifu Wateja wake waliositishiwa huduma sababu ya madeni ya bili za maji kufika ofisi za Mamlaka zinazowahudumia ili kuingia mkataba wa kulipa madeni yao na kurejeshewa huduma bila faini ya Shilingi 15,000
Wahi sasa unufaike na ofa hii maalum ambayo imeanza tarehe 9.5.2025 hadi 31.5.2025
Kwa maelezo zaidi, wasiliana nasi kupitia kituo cha huduma kwa wateja 0800110064 (Bila malipo) au 0735202121 (WhatsApp tu)
Imetolewa na
Kitengo cha Mawasiliano