TAARIFA KWA UMMA - TAARIFA YA KUKOSEKANA KWA HUDUMA YA MAJI KWA WAKAZI WA BAGAMOYO HADI ILALA

TAARIFA KWA UMMA
TAARIFA YA KUKOSEKANA KWA HUDUMA YA MAJI KWA WAKAZI WA BAGAMOYO HADI ILALA
19.08.2025
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) inawajulisha Wananchi wanaohudumiwa kupitia Mtambo wa uzalishaji Maji Ruvu Chini kuwa, kutakuwa na maboresho yatakayoathiri upatikanaji huduma ya Maji kwa wastani wa Saa 12
Muda: Siku ya Alhamisi, Agosti 21,2025 kuanzia Saa 1 Asubuhi hadi Saa 12 Jioni
Sababu: Kuruhusu maboresho ya kawaida ya Miundombinu katika Mtambo wa Ruvu Chini
Maeneo yatakayoathirika ni;
Bagamoyo, Mapinga, Mabwepande, Bunju, Tegeta, Mbweni, Boko, Kunduchi, Salasala, Goba, Madale, Mbopo, Mivumoni, Kawe, Lugalo, Makongo, Chuo-Kikuu Dar es Salaam (UDSM), Mwenge, Kijitonyama, Mikocheni, Msasani, Oysterbay, Masaki, hospitali ya Taifa Muhimbili, Mwananyamala, Kinondoni, Magomeni, Kigogo, Chang'ombe, Keko, Kurasini, Kiwalani, llala na katikati ya Jiji
Kukamilika kwa maboresho haya kutaimarisha kiwango cha uzalishaji na usambazaji Maji kwa Wananchi wanaohudumiwa na Mtambo huu.
Mamlaka inaomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza na inawasihi Wananchi kuhifadhi maji ya kutosha ili kukidhi mahitaji muhimu kipindi cha matengenezo.
Kituo cha huduma kwa wateja: 0800110064 (Bila malipo) na 0735 202121 (WhatsApp tu)
Everlasting Lyaro
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano
DAWASA