Wizara ya Maji

Dar es Salaam Water Supply And Sanitation Authority (DAWASA)

TIRA Logo
TAARIFA KWA UMMA - UHAKIKI NA UBORESHAJI WA TAARIFA ZA WATEJA
18 Jun, 2025 Pakua
TAARIFA KWA UMMA - UHAKIKI NA UBORESHAJI WA TAARIFA ZA WATEJA

TAARIFA KWA UMMA

UHAKIKI NA UBORESHAJI WA TAARIFA ZA WATEJA

17.6.2025

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) inawatangazia Wateja wake wote katika Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani kuwa, inaendelea na zoezi la uhakiki na uboreshaji wa taarifa za wateja kwa lengo la kuendelea kuimarisha Mawasiliano kati ya Mamlaka na wateja.

Zoezi hili litahusisha upokeaji wa taarifa za wateja ambao wanapata huduma za Majisafi na Majitaka na hawapokei ujumbe wa ankara kutoka DAWASA.

Taarifa hizi ziwasilishwe kuanzia Tarehe 18.6.2025 hadi 30.6.2025 kwa kutuma ujumbe au kupiga simu namba 0749 000 555 (Taarifa zitakazopokelewa zitalindwa) au kuwasilisha taarifa hizo katika Ofisi za DAWASA zilizo karibu.

Kumbuka Malipo yote ya huduma za DAWASA hufanywa kupitia Mfumo wa Malipo ya Serikali kwa kutumia Kumbukumbu Namba (Control namba)

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano - DAWASA