TAARIFA KWA UMMA - USOMAJI MITA ZA MAJI DAR ES SALAAM NA PWANI KUANZA JUNI 10 - 15, 2025
							
							
							
							
							
						
					
                            
                                 09 Jun, 2025
                            
                                                        
                                 Pakua
                            
                                                    
                    
                    TAARIFA KWA UMMA
USOMAJI MITA ZA MAJI DAR ES SALAAM NA PWANI KUANZA JUNI 10 - 15, 2025
9.06.2025
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) inawaatarifu Wateja na Wananchi katika Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani, kuwa zoezi la usomaji mita za maji linaanza Juni 10 hadi 15, 2025.
Baada ya zoezi la usomaji mita kukamilika, Mteja atapokea ujumbe wa kuhakiki usomaji wa mita yake kabla ya bili kutumwa.
Kwa taarifa zaidi wasiliana nasi kituo cha huduma kwa wateja 0800110064 (Bure) na 0735 202121 (WhatsApp tu)
Imetolewa na 
Kitengo cha Mawasiliano
            