TAARIFA KWA UMMA - USOMAJI MITA ZA MAJI DAR NA PWANI KUANZA AGOSTI 10-15, 2024
10 Aug, 2024
Pakua
TAARIFA KWA UMMA
USOMAJI MITA ZA MAJI DAR NA PWANI KUANZA AGOSTI 10 -15, 2024
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) inawataarifu wateja na wananchi katika mikoa ya Dar es Salaam na Pwani, kuwa zoezi la usomaji wa mita za maji utaanza Agosti 10 hadi 15, 2024.
Mamlaka inaomba ushirikiano kwa Wananchi pindi watoa huduma wa DAWASA watakapopita kutekeleza zoezi hili.
Baada ya zoezi la usomaji mita kukamilika, Mteja atapokea ujumbe wa kuhakiki usomaji wa mita yake kabla ya bili kutumwa.
Kwa taarifa zaidi wasiliana nasi kituo cha huduma kwa wateja 0800110064 (Bure) na 0735-202121 (WhatsApp tu)
Imetolewa na
Kitengo cha Mawasiliano