Wizara ya Maji

Dar es Salaam Water Supply And Sanitation Authority (DAWASA)

TIRA Logo
TAARIFA KWA UMMA - USOMAJI MITA ZA MAJI DAR NA PWANI KUANZA JULAI 10 - 15, 2024
09 Jul, 2024 Pakua

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) inawataarifu wateja na wananchi katika mikoa ya Dar es Salaam na Pwani, kuwa zoezi la usomaji wa mita za maji utaanza Julai 10 hadi 15, 2024.

Mamlaka inaomba ushirikiano kwa watoa huduma wa DAWASA pindi watakapopita katika makazi yenu kutekeleza zoezi hili. 

Baada ya zoezi la usomaji mita kukamilika, Mteja atapokea ujumbe wa kuhakiki usomaji wa mita yake kabla ya bili kutumwa.

Kwa taarifa zaidi wasiliana nasi kituo cha huduma kwa wateja 0800110064 (Bure) na 0735-202121 (WhatsApp tu)

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano.