TAARIFA KWA UMMA - ZOEZI LA KUHAMISHA WATEJA KUPISHA MATENGENEZO YA BARABARA

TAARIFA KWA WAKAZI WA TEGETA
ZOEZI LA KUHAMISHA WATEJA KUPISHA MATENGENEZO YA BARABARA
10.10.2025
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) inawatangazia wateja na eneo la Tegeta kwa Ndevu hadi Pieta katika Kata ya Kunduchi Wilaya ya Kinondoni kuwa, kutakua na ukosefu wa huduma ya maji kwa muda wa Saa Saba siku ya Ijumaa tarehe 10.10.2025
Muda; Saa 3 Asubuhi hadi Saa 10 jioni
Sababu; Kuruhusu zoezi la kuhamisha mtandao wa Maji wa Wananchi ili kuruhusu ujenzi wa barabara.
Maeneo yatakayoathirika ni;
Tegeta kwa Ndevu, Mzumbe, Kontena, Club Ngo'mbe, T mark, Triple J pamoja na Pieta
Tunaomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza.
Wasiliana nasi Kituo cha huduma kwa wateja 181, 0800110064 (bure) na 0733 451 861 (DAWASA Tegeta)
Imetolewa na
Kitengo cha Mawasiliano