TAARIFA KWA WAKAZI WA KIBAHA HADI KISARAWE - Kuzimwa kwa mtambo wa Maji Ruvu Juu kwa Saa 15
15.7.2024
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) inawatangazia Wateja na Wananchi wanaohudumiwa na mtambo wa kuzalisha Maji Ruvu Juu kuwa, kutakuwa na ukosefu wa huduma ya maji siku ya Jumanne Julai 16 ,2024 kwa muda wa saa 15 kuanzia Saa 12 asubuhi hadi Saa 3 usiku.
Sababu: Kuruhusu matengenezo kwenye bomba kuu la kusafirisha Maji ghafi kutoka Mtoni kwenda Mtamboni katika eneo la Mlandizi.
Maeneo yanayoathirika ni;
Ruvu darajani, Ruvu JKT, Mlandizi, Mbwawa, Visiga, Mile 35, Misugusugu, Kongowe, Soga, Miembe Saba, Kwa Mfipa, Mwendapole, Tanita, Kwa Mathias, Kwa Mbonde, Picha ya Ndege, Lulanzi, Kibaha, Kiluvya, Kibamba, Mbezi, Magari Saba, Mbezi Inn, Mshikamano, Mbezi, Kimara,Tabata, Kinyerezi, Kisukuru, Msigani, Maramba Mawili, Tabata, Kimara B, Kimara Korogwe, Bucha, Baruti, Ubungo, Ukonga, Pugu, Gongo la Mboto, Uwanja wa Ndege, Majumba sita , Kiwalani, Segerea, Kinyerezi na Kisarawe.
Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.
Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kupitia kituo cha huduma kwa wateja
0800110064 (bure) au
0735 202 121(WhatsApp tu)
Imetolewa na
Kitengo cha Mawasiliano