TAARIFA KWA WAKAZI WA KIBAMBA - MABORESHO MIUNDOMBINU YA UMEME YATAKAYOATHIRI UPATIKANAJI HUDUMA YA MAJI

TAARIFA KWA WAKAZI WA KIBAMBA
MABORESHO MIUNDOMBINU YA UMEME YATAKAYOATHIRI UPATIKANAJI HUDUMA YA MAJI
16.10.2025
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) inawataarifu Wananchi katika eneo la Kibamba hadi Mpiji Magoe Wilaya ya Ubungo kuwa, kutakua na ukosefu wa huduma ya maji kwa muda wa Saa Saba siku ya Alhamisi tarehe 16.10.2025
Muda: Kuanzia saa 4 Asubuhi hadi Saa 11 jioni
Sababu ; Kuruhusu Maboresho ya umeme katika Wilaya ya Kibaha yatakayoathiri upatikanaji wa umeme katika kituo cha kusukuma maji Kibamba kinachohudumia wakazi wa maeneo tajwa.
Maeneo yatakayoathirika ni;
Kibamba, Kibwegere, Delini, Hondogo, Mpiji Magohe, Kibesa, Msakuzi, Muongoni, Makabe, Msumi, Mdidimua, Kwa Lipenya, Mnarani Kwa Paulo, Rising Star, Kwa mkapa, Kwa Lubaba, na Magufuli Stand
Tunaomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza.
Wasiliana nasi Kituo cha huduma kwa wateja 181 (bure) na 0734 460 022 (DAWASA Kibamba)
Imetolewa na
Kitengo cha Mawasiliano
DAWASA