TAARIFA KWA WAKAZI WA MBEZI JUU - MABORESHO YA DHARURA YATAKAYOATHIRI UPATIKANAJI HUDUMA YA MAJI

TAARIFA KWA WAKAZI WA MBEZI JUU
MABORESHO YA DHARURA YATAKAYOATHIRI UPATIKANAJI HUDUMA YA MAJI
26.6.2025
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) inawajulisha Wananchi wa Mbezi juu katika maeneo ya Jogoo, Baraza la Mitihani, St. Marry's na Vosel) kuwa kutakuwa na ukosefu wa huduma ya Maji kwa wastani wa Saa 24 kupisha matengenezo ya dharura.
Muda: Alhamisi, Juni 26, 2025 Saa 5 usiku hadi Ijumaa, Juni 27, 2025 kuanzia Saa 5 usiku.
Sababu: Kuruhusu maboresho dharula katika mfumo wa kusukuma Maji eneo la Mbezi juu Jogoo.
Maeneo yatakayoathirika ni;
Baraza la Mitihani, VOSEL Hotel, Mashine ya zamani, Bar mpya, Twiga street, Kanisa la Sabato, 34 street, Asante Grey, Mzee Lema, Msafiri street na Chongolo street.
Tunaomba radhi kwa usumbufu utakao jitokeza.
Kwa mawasiliano zaidi wasiliana nasi Kituo cha huduma kwa wateja 0800110064 (Bila Malipo) na 0735 202 121 (WhatsApp tu)
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano - DAWASA