TAARIFA KWA WAKAZI WA TEGETA - MATENGENEZO YA DHARURA YATAKAYOATHIRI UPATIKANAJI WA HUDUMA
							
							
							
							
							
						
					
                            
                                 23 Oct, 2025
                            
                                                        
                                 Pakua
                            
                                                    
                    
                    TAARIFA KWA WAKAZI WA TEGETA
MATENGENEZO YA DHARURA YATAKAYOATHIRI UPATIKANAJI WA HUDUMA
23.10.2025
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) inawataarifu  Wateja na Wananchi wa maeneo ya Tegeta Nyuki hadi Chatembo kuwa, kutakua na ukosefu wa huduma ya maji kwa muda wa saa 7 leo, Oktoba 23, 2025
Muda; Saa 5 Asubuhi hadi Saa 12 jioni
Sababu ; Kuruhusu matengenezo ya dharura katika chanzo cha bomba linalohudumia maeneo hayo.
Maeneo yatakayoathirika ni; 
Tegeta Nyuki, Umeme wa Zanzibar, Bahari Beach, Nyota Njema, Pwani, Machakani, Kondo, Namanga, Magereji na Chatembo
Tunaomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza.
Wasiliana nasi:
Kituo cha huduma kwa wateja 181 (bure) na 0737 730523 (DAWASA Tegeta)
 
            