TAARIFA MUHIMU - BADO SIKU 1 KUISHA KWA OFA MAALUM
31 May, 2025
Pakua

TAARIFA MUHIMU
BADO SIKU 1 KUISHA KWA OFA MAALUM
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) inawakumbusha Wananchi na wateja wake kuwa, bado Siku Moja kuisha kwa ofa maalum ya kutolipa faini ya kurejeshewa huduma (Reconnection fee)
DAWASA inawasisitiza Wateja wote waliositishiwa huduma sababu ya madeni ya bili za Maji kufika katika ofisi za Mamlaka wanazohudumiwa ili kuingia mikataba ya kulipa madeni na kurejeshewa huduma bila fainiya Shilingi 15,000.
Mwisho wa ofa hii ni Mei 31, 2025.
Kwa Mawasiliano zaidi, wasiliana nasi Kituo cha huduma kwa Wateja 0800110064 (Bila Malipo) au 0735 202 121 (WhatsApp tu).
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano