TAARIFA MUHIMU - KURUHUSU HUDUMA YA MAJI KWA WAKAZI WA BANGULO HADI SEGEREA
17 Dec, 2025
Pakua
TAARIFA MUHIMU
KURUHUSU HUDUMA YA MAJI KWA WAKAZI WA BANGULO HADI SEGEREA
Ndugu wateja mnaohudumiwa kupitia TANKI LA BANGULO tunapenda kuwajulisha kuwa tumefungulia huduma ya maji, maeneo yafuatayo yatapata huduma;
Segerea, Migombani, Mangumi, Undewani, Maxmilian, Seminary, Tototundu, Chama, Kwa Mgonja, Segerea Stendi, Genius Kings, Zahanati ya Segerea, Majimaji Street, Makongoro Mahanga na Mazongera.
Kumbuka kuwa na hifadhi ya kutosha ya vyombo vya Maji kipindi hiki cha upungufu
Kwa changamoto ya huduma tupigie 181 (Bure)
