TAARIFA MUHIMU - TUMEFUNGULIA HUDUMA KUPITIA TANKI LA KIMARA
11 Dec, 2025
Pakua
TAARIFA MUHIMU
TUMEFUNGULIA HUDUMA KUPITIA TANKI LA KIMARA
Ndugu Mteja mnaohudumiwa kupitia TANKI LA KIMARA tunapenda kuwajulisha kuwa tumefungulia huduma ya maji maeneo yafuatayo yatapata huduma;
Kata ya Kimara katika maeneo ya;
Kimara Mid-Land, Baruti 770, Baruti 800, Kilungule A na B, Makoka, Unyamwezini, Kings na Golani.
Kata ya Ubungo
City View na Novo (Kwa baadhi ya maeneo).
Maeneo yatakayopata huduma kupitia Mgao wa nyuma ya Matenki ya Kimara ni; Matangini, Stopover, Kimara B, Mkwajuni, Saranga, Kwa Msuguri, Temboni, Malamba mawili, Msigani, Kanisa la Udongo, King'ong'o na Michungwani.
Kumbuka kuwa na hifadhi ya kutosha ya vyombo vya Maji kipindi hiki cha upungufu.
KWA CHANGAMOTO TUPIGIE 181 (BURE)
